BAADA ya kuambulia kichapo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, matajiri wa Dar Azam FC wameanza maandalizi.
Ni Mzizima Dabi ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 3-2 Azam FC ambapo Aziz Ki aliandika rekodi ya kufunga hat trick katika mchezo huo.
Mabao ya Azam FC inayonolewa na Yusuph Dabo yalifungwa na Gibril Sillah na Prince Dube.
Ni Oktoba 27 2023 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.