MO AWEKA MEZANI ZAIDI YA 500M

Kuelekea mchezo huo, unaambiwa wachezaji wa Simba wamechachamaa wakiitaka shilingi milioni 500 walizoahidiwa na Rais wa Heshima wa Klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’ akiwataka kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Chanzo chetu kutoka Simba, kimeliambia Spoti Xtra kwamba, kabla ya Simba kuanza safari kuelekea Misri, Mo alikutana na wachezaji vyumbani kwenye Dimba la Mkapa na kuwawekea kitita cha shilingi milioni 500 mezani kama watafanikiwa kushinda dhidi ya Al Ahly.

“Mo alitoa ahadi yake mapema tu kabla ya mchezo wa kwanza pale kwa Mkapa ambapo aliwaambia wachezaji kama watashinda mchezo huo, basi atawapa shilingi milioni 500 ikiwa ni sehemu ya hamasa yake, huku akiwaambia zile posho za siku zote zitabaki kama kawaidi, hivyo kama tukishinda katika mchezo wa marudiano, kuna zaidi ya shilingi milioni 500 wachezaji watapata,” kilisema chanzo hicho.