AZAM FC MBELE YA YANGA HAWANA BAHATI KABISA

KATIKA mechi mbili za ushindani ndani ya dakika 180, matajiri wa Dar Azam FC hawana bahati kabisa mbele ya Yanga.

Katika mchezo wa kwanza kumenyana ilikuwa Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 2-0 Azam FC.

Ngoma ikawa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Mkapa dakika 90 ubao ulisoma Yanga 3-2 Azam FC.

Ndani ya dakika 180 Azam FC imetunguliwa mabao matano na Yanga huku wao wakigotea kufunga mabao mawili pekee.

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi sita huku Azam ikigotea nafasi ya tatu na pointi 13.

Aziz KI ni namba moja kwa nyota wenye mabao mengi akiwa nayo sita kibindoni msimu wa 2023/24.