Skip to content
MZIZIMA Dabi inapigwa Oktoba 23,2023 Uwanja wa Mkapa kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu baada ya dakika 45.
Dakika 45 za mwanzo timu zote zinakwenda bao ulikuwa unasoma 1-1.
Ni Aziz KI alianza kufunga kwa Yanga dakika ya 8 akimtungua Idrissu Abdulai na bao la usawa kwa Azam FC limefungwa na Gibrril Sillah dakika ya 19.
Djigui Diarra mdaka mishale alikwama kuokoa hatari hiyo ya mpigaji aliyekuwa nje ya 18 na kuruhusu bao la kuweka usawa kipindi cha kwanza cha mchezo.
Kipindi cha pili Yanga wamefunga mabao mawili kupitia kwa Aziz KI na Azam FC bao moja kupitia kwa Prince Dube.