MZIZIMA Dabi imezizima Uwanja wa Mkapa hukuAzam FC wakiwa mashuhuda wakiyeyusha pointi tatu mbele ya wapinzani wao Yanga.
Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Azam FC kupoteza kwa msimu wa 2023/24 kwenye mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.
Baada ya dakika 90 kumeguka ubao umesoma Yanga 3-2 Azam FC katika msako wa poiñti tatu muhimu.
Ni Aziz Ki nyota wa Yanga kajaza kimiani mabao matatu, hat trick yake ya kwanza msimu wa 2023/24.
Ni dakika ya 8, 69 na 72 kamtungua Idrissu Abdulai ambaye alikwama kuokoa hatari hizo.
Kwa Azam FC ni Gibril Sillah dakika ya 19 na Prince Dube dakika ya 62 kwa mkwaju wa penalti