MAPUNGUFU YA SIMBA AFL YAFANYIWE KAZI

UBORA wa kikosi cha Simba ambao unazungumzwa kwenye midomo na mashabiki pamoja na viongozi ni vitu viwili ambavyo vinafikirisha.

Haina maana kwamba wachezaji wa Simba sio bora hapana, mwendo wa makosa kwenye mechi wanazocheza unakwenda kujirudia mara kwa mara.

Tumeona namna ambavyo waliondolewa katia hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na Wydad Casablanca ugenini. Makosa ilikuwa ni washambuliaji kukwama kumalizia nafasi wanazotengeneza na safu ya ulinzi kushindwa kulinda ushindi wao.

Mwisho ikabaki historia kuwa Simba iliondolewa hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mikwaju ya penalti, huu ni wimbo ambao unapaswa ubadilike kwa wakati huu.

Kwa mara nyingine tena, Simba ilipata fursa ya kuwa nyumbani kwenye mchezo wa ufunguzi wa African Football League, Uwanja wa Mkapa dhidi ya Al Ahly ambapo dunia ilishuhudia namna burudani ilivyokuwa.

Mwisho walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 ilihali mwanzo kila mmoja alikuwa anatamba kwamba wanakwenda kushinda nyumbani.

Kazi inaweza kuishia Uwanja wa Mkapa ikiwa safu ya ushambuliaji, viungo na mabeki hawatakuwa na ushirikiano kwenye kutimiza majukumu yao kwa wakati.

Al Ahly huwa wanakuwa tofauti wakiwa nyumbani hilo wanalitambua Simba kwa kuwa katika mechi za kimataifa hivi karibuni hawakupata nafasi ya kushinda kwenye mechi walizokutana.

Nafasi nyingine ya kupambana na kushirikiana kufanyia kazi makosa ili hatua ya robo fainali isiwe ni wimbo wa Simba kila leo.

ReplyForward