KUELEKEA Mzizima Dabi, Oktoba 23,2023 uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa wanatambua utakuwa ni mchezo mgumu kutokana na aina ya wachezaji waliopo ndani ya kikosi cha Azam FC.Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga amesema kuwa wanatambua aina ya wachezaji watakaokutana nao kwenye mchezo huo kuwa ni bora.
“Wapinzani wetu Azam FC wana wachezaji wazuri ambao wengi hawaa uoga kwa mechi kubwa hilo tunalitambua hivyo maandalizi yanafanyika kwa umakini kuelekea mchezo wetu.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi hasa ukizingatia tutakuwa Uwanja wa Mkapa na tunajua kwamba hii ni burudani kwenye ligi ni muda wa kuendelea kuishangilia timu ili kuwapa nguvu wachezaji,”.
Yanga imecheza mechi tano na kupoteza mchezo mmoja, Azam FC kwenye mechi tano za ligi haijapoteza.