HAPA NDIPO SIMBA WALIPOFANYA MAKOSA DHIDI YA AL AHLY

MPIRA ni mchezo wa makosa hilo lipo wazi na ilikuwa hivyo kwenye mchezo wa ufunguzi wa Afrinca Football League kati ya Simba dhidi ya Al Ahly.

Dakika 45 za mwanzo kwa wachezaji wa Simba walionekana kuumiliki mpira bila kuwa na mpango na mwisho walitunguliwa bao moja na Slim dakika ya 45.

Angalau kidogo kipindi cha pili walianza kwa kasi wakiwa na mipango na kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Kibu Dennis kisha bao la pili likafungwa na Sadio Kanoute.

Bao hilo lilileta hasira kwa Al Ahly ambao walipata bao dakika tatu mbele kupitia kwa Karhaba na mwisho ubao wa Uwanja wa Mkapa ukasoma Simba 2-2 Al Ahly.

Legend, Jembe kwenye masuala ya habari za michezo ameweka wazi kuwa makosa ya Simba yaliwaadhibu namna hii:-

“Makosa waliyofanya Simba na hasa pembeni, yamewaadhibu na wao wametumia makosa machache ya Al Ahly kufunga mabao mawili.

“Bila shaka ni mechi bora ya ufunguzi wa michuano ya African Football League na mbele ya Rais wa   Fifa, Gianni Infantino na Rais wa Caf, Patrice Motsepe pia kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger.

“WAMEONYESHA WANASTAHILI kuwa kwenye AFL na wamestahili kuleta uzinduzi huo ufanyike jijini Dar es Salaam NYUMBANI kwa Simba.

Mpira wa Tanzania unapiga hatua lakini bado tuna safari ndefu….Simba wajipange kwa mechi ijayo,”.