Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe ameweka wazi kuwa msimu ujao kutakuwa na timu shiriki 24 kwenye African Football League ambayo inatarajiwa kufunguliwa rasmi leo Oktoba 20, 2023.
Ni ardhi ya Tanzania, Uwanja wa Mkapa umepata fursa ya kuzindua mashindano hayo makubwa ambayo yanafuatiliwa na wengi duniani yakifanyika kwa mara ya kwanza.
Simba itamenyana na Al Ahly kwenye mchezo wa leo ambapo mashabiki wengi wamejitokeza pamoja na wageni mbalimbali wa kitaifa na kimataifa.
“Nawashukuru viongozi wa timu zote nane zinazoshiriki michuano ya African Football League pamoja na zile 24 ambazo zitashiriki mwakani.
“Msimu ujao tutakuwa na timu 24 kwenye michuano ya African Football League tutazipata kupitia ranki za CAF pamoja na mafanikio yake katika ligi za nyumbani,