SIMBA YATOSHANA NGUVU NA AL AHLY

MCHEZO wa African Football League ambao ni wa ufunguzi Simba imetoshana nguvu na Al Ahly.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Simba 2-2 Al Ahly.

Mabao ya Simba yamefungwa na Kibu Dennis na Sadio Kanoute huku yale ya Al Ahly yakifungwa na Slim na Kahraba kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Simba watajilaumu wenyewe kwenye safu ya ulinzi kwa kukwama kuokoa hatari katika mchezo huo.