KIGONGO CHA KWANZA CHA KOCHA MPYA SINGIDA FOUNTAIN GATE

RICARDO Ferreira, Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho kwenye mchezo wa ligi dhdi ya Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa, utakaochezwa Jumamosi.

Kikosi cha Singida Fountain Gate kimewasili Ruangwa salama salmini kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni Meddie Kager, Beno Kakolanya, Gadiel Michael.

Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Masanza amesema kuwa kocha huyo yupo tayari kwa mchezo huo utakaokuwa na ushindani mkubwa wakizitaka pointi tatu.

“Benchi la ufundi limeanza kazi kwa ajili ya mechi zetu na tunahitaji kupata pointi tatu muhimu. Mchezo wetu dhidi ya Namungo kocha wetu mpya ataanza kazi yake akiwa anatambua kwamba aina ya kikosi kilichopo ni bora na amefurahia kuwaona kwenye uwanja wa mazoezi.

“Kikubwa mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwani baada ya mchezo huu tutakuwa na mchezo mwingine mgumu dhidi ya Yanga,”