UKIWA ni mchezo wa ufunguzi wa African Football League, mashabiki wa Simba wameshuhudia namna mbinu za Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kikiwa nyuma.
Dakika 45 ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Simba 0-1 Al Ahly
Mtupiaji kwenye mchezo huo ambao una ushindani mkubwa kwa timu zote ni Reda Slim aliyetumia makosa ya safu ya ulinzi ya Simba kwa kupachika bao hilo dk 45+1.
Majalo ya beki Shomari Kapombe, Mohamed Hussein yamekwama kuleta matunda kwa Simba kipindi cha kwanza.
Ni Ally Salim ameanza langoni kwenye mchezo wa leo huku Ayoub Lakred akiwa benchi akisoma mchezo.