UTUZANJI UWANJA WA MKAPA NI WA KILA MMOJA

GHARAMA kubwa zimetumika katika kuuboresha Uwanja wa Mkapa hilo lipo wazi. Kwa kuwa kila kitu inaonekana kuwa bora kwa wakati huu kuanzia sehemu ya kuchezea mpaka viti.

Ikumbukwe kwamba hii ni awamu ya kwanza ya maboresho. Kila mmoja aliyehusika kwa namna moja ama nyingine anastahili pongezi kwa jambo hilo ambalo amelifanya.

Simba itakuwa timu ya kwanza kuutumia uwanja huo baada ya maboresho kwenye mechi ya ushindani. Uwanja wa Mkapa ulifungwa kwa muda na ulikuwa hautumiki kwenye mechi kubwa za ushindani.

Maboresho ambayo yamefanywa yanatoa fursa kwa timu kubwa na ndogo kupata nafasi ya kucheza hapo. Hilo lipo wazi hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni mwendelezo wa matuzo kwa watumiaji.

Isiwe ni mchezo wa Simba dhidi ya Al Ahly ripoti zikarejea kuwa zaidi ya viti 10 vimeharibiwa ilihali matengenezo yapo kwenye awamu ya kwanza.

Utunzaji wa vifaa vyote ambayo vipo ndani ya Uwanja wa Mkapa ni jukumu la kila mmoja kwa wakati huu atakeyekuwa ndani ya uwanja nan je ya uwanja.

Wapo ambao wanashambulia kuhusu maboresho ya uwanja kwa kudhani ni kitu cha kawaida kimefanyika hapo. Haiwezi kuwa maboresho ya kawaida kwa ajili ya mechi kubwa hapana ukweli uwekwe bayana kuwa maboresho yaliyofanyika ni makubwa.

Kila la kheri wageni na wenyeji kwenye utunzani wa miondombinu iliyofanyiwa maboresho makubwa Uwanja wa Mkapa.