MAJEMBE YA GAMONDI YANGA HAYA HAPA

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga katika kikosi chake ana majembe mawili ya kazi yanayompa kiburi cha kuwa imara kwenye upande wa ulinzi kutokana na kuwapa nafasi mara kwa mara.

Katika Ligi Kuu Bara, Yanga kwenye mechi tano ilizocheza ilitunguliwa mabao mawili pekee ubao wa Uwanja wa Highland Estate ulisoma Ihefu 2-1 Yanga, bao la Yanga lilifungwa na Pacome Zouzoa dakika ya tatu.

Ni Dickson Job ni chaguo la kwanza la Gamondi kwenye mechi zote za ligi alianza na kuandika rekodi ya kukomba dakika zote 450 kwa kuwa alikuwa akianza mwanzo mwisho.

Mbali na kucheza mechi zote Job ni mfungaji wa bao la kwanza ndani ya kikosi cha Yanga msimu wa 2023/24 alipowatungua KMC mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Nyota wa pili ni Yao Attohuula ambaye kapata zali la kucheza mechi zote tano na kukomba dakika 388, kibindoni katupia bao moja pia.

Gamondi amesema kuwa wachezaji wote wanaonyesha uwezo katika eneo la mazoezi pamoja na sehemu ya mchezo husika.

“Kila mchezaji anaonyesha uwezo wake kwenye eneo la mazoezi na eneo la mechi hivyo tutazidi kupambana kupata matokeo chanya kwenye mechi zetu,” amesema Gamondi.