RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa zawadi ya Tsh. 10 milioni kwa kila bao ambalo litafungwa na Simba.
Huo ni mchezo wa African Football League ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 20,2023.
Samia ameahidi kuwa kwa bao moja ambalo litafungwa katika mchezo wa African Football League dhidi ya Al Ahly ambao utachezwa siku ya Ijumaa, Oktoba 20, 2023 saa 12:00 jioni Uwanja wa Mkapa.
Simba inanolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ipo kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Miongoni mwa vitu ambavyo vimefanyiwa kazi kwa ukaribu ni pamoja na maboresho ya Uwanja wa Mkapa ambao kwa namna moja umekuwa katika muonekano wa kipekee.
Hiyo yote ni maboresho katika awamu ya kwanza ya Uwanja wa Mkapa.