KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha Parimatch imeamua kuwapa fursa mpya wateja wake kwa kucheza Casino kiganjani ambayo imesheheni zaidi ya michezo 200 mikali ndani yake ikiwemo BINGO ambayo imeshika kasi kwa kupendwa na watu wengi.
Hayo yamebainishwa na Ofisa Habari wa Parimatch Tanzania, Ismael Mohamed jijini amesema kwamba kupitia tovuti yao ya Parimatch wataweza kufurahia kucheza na kushinda michezo mingi ya Bingo kwa dau dogo la kuanzia shilingi 250.
“Hakuna haja tena ya kuendelea kusubiria hadi ligi zirudi upya ndio utengeneze pesa kwa kubeti kwenye soka, sisi kama Parimatch tumeamua kuwaletea Casino yenye michezo zaidi ya 200 tofauti tofauti yenye kukupa msisimko ambao hujawahi kuupata hapo awali.
“Kwa mfano unaweza kucheza mchezo wa Bingo instant kwa dau la Shilingi 250 na kila sekunde watu wanavuna mkwanja wa
maana yaani huu sio utani watu wanapiga kiukweli”, amesema Ismael.
Aidha, Ismael aliendelea kwa kusema kwamba “Utofauti wa Casino ya Parimatch unaanzia kwenye ubora wa mfumo wetu ambao unaendeshwa kisasa zaidi na kuwezesha kupata malipo kwa haraka zaidi sekunde chache tu mara tu unaposhinda,” .
Pamoja na hayo, Ismael aliwasisitizia wadau wa Parimatch kuendelea kufurahia kucheza Virtual games na michezo mingine mbalimbali kupitia tovuti yao ambayo itaweza kuwaburudisha na kusisimua katika kipindi hiki cha kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa ligi mbalimbali ulimwenguni.
Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya Ukaribisho ya 125% hadi kufikia TZs 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao!
Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa
huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za
kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka, kampuni ya
Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa
vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.