JEMBE LILILOKUWA LINAWINDWA YANGA SAFARI KUMKUTA

INAELEZWA kuwa Francis Kazadi mshambuliaji wa Singida Fountain Gate huenda akapigwa panga katika dirisha dogo.

Kazadi alikuwa anatajwa kuwa katika rada za Yanga mwisho akaibukia Singida Fountain Gate.

Kwa msimu wa 2023/24 hajapata zali la kufunga kwenye mechi za ligi hivyo bado anajitafuta kuonyesha makali yake ndani ya timu hiyo.

Nyota huyo alionyesha uwezo mkubwa katika Kombe la Mapinduzi alipoibuka mfungaji Bora alipofunga mabao sita katika Ligi Kuu Bara mambo yamekuwa magumu kwake.

Alisajiliwa akiwa huru baada ya kuachana na Al Masry ya Misri aliwahi kucheza AS Vita , DC Motema Pembe kwa nyakati tofauti.