MASTAA WAPIGWA MKWARA YANGA

INATAJWA kuwa mastaa wote waliopo kikosi cha Yanga ikiwa  ni pamoja na nyota watano ndani ya kikosi cha Yanga wameambiwa wanapaswa kuonyesha uwezo wao kwenye mechi zao zijazo ili kuendelea kupata namba katika kikosi hicho.

Yanga chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi imecheza mechi tano za Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya tatu na pointi zake kibindoni ni 12.

Mchezo wao unaofuata kwenye ligi ni dhidi ya Azam FC unatarajiwa kuchezwa Oktoa 25.

Mastaa ambao hawajapa namba kwenye mechi za hivi karibuni ni pamoja na Crispin Ngushi ambaye aliibuka hapo kutokà Mbeya Kwanza, Hafiz Konkon hajawa na uhakika kikosi cha kwanza , Aboutwalib Mshery, Gift Fred na Dennis Nkane.

Nkane amekuwa na zali lakuanzia benchi na kupata nafasi ya kucheza kwenye mechi za ligi licha ya kushindwa kuonyesha makeke yake uwanjani.

Taarifa zimeeleza kuwa mastaa hao wanapaswa kuongeza nguvu sehemu ya mazoezi na wakipata nafasi wanapaswa kufanya kweli.

Hivi karibuni Gamondi alisema kuwa kila mchezaji aliyepo ndani ya Yanga ana uwezo mkubwa na watapata nafasi ya kucheza.