PANAPOVUJA PAMEONEKANA NI MUDA WA KUJIPANGA UPYA

BAADA ya mechi tano za Ligi Kuu Bara kuchezwa tayari pale ambapo panavuja pameshatambulika. Makosa ya timu kwenye dakika 90 yalionekana na benchi la ufundi liliona hivyo ni muda wa kufanyia kazi.

Wapo ambao lawama wanazikimbiza kwa waamuzi, hili nalo linapaswa kufanyiwa kazi. Wachezaji nafasi zile za dhahabu wanazozipata ni muhimu kuzitumia.

Kawaida kila baada ya mchezo kila mmoja anatafuta mchawi nani. Muda uliopo kwa sasa ni muhimu kuanza kufanyia kazi mapungufu ili kuwa bora wakati ujao ligi itakaporejea.

Zipo timu ambazo hazijapata ushindi kwenye mechi walizocheza ni muhimu kufanya maandalizi kwa mechi zijazo kupata matokeo.

Inawezekana kuna mahali ambapo walikwama kutokana na kushindwa kuwa na muda wa maandalizi. Lakini kwa sasa ni muhimu kufanya kazikwa umakini kupata matokeo kwenye mechi zijazo.

Mzunguko wa kwanza una ushindani mkubwa na huu unatoa picha kuelekea mzunguko wa pili. Kabla ya kufika mzunguko wa kwanza ni muhmu kufanya kazi kubwa wakati huu kupata matokeo mazuri.

Kila kitu kinawezekana kwa kufanyia kazi yale mapungufu, lawama hazileti matokeo mazuri bali kujituma na kuwa makini katika kutumia nafasi.

Muda hausubiri na hakuna muda wa ziada kwa kuwa bado kuna muda wa kufanyia kazi makosa iwe hivyo kwa timu zote zinazoshiriki ligi.