Skip to content
UBAO wa Uwanja wa Liti umesoma Singida Fountain Gate 1-2 Simba ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Bao la uongozi kwa Simba limepachikwa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 26 lililomshinda Beno Kakolanya.
Ni pasi ya Kibu Dennis ambaye amekuwa kwenye dakika 45 bora za kipindi cha kwanza ugenini.
Deus Kaseke ni yeye aliweka usawa dakika ya 52 huku bao la ushindi likifungwa na Moses Phiri dakika ya 82 likiwa ni bao lake la kwanza ndani ya ligi.