WAAMUZI HAKI MUHIMU KUZINGATIA KWENYE MAAMUZI

TARATIBU dawa inazidi kuingia kwenye kidonda ambacho kinaendelea kupona. Licha ya kuendelea kwa maumivu ambayo mgonjwa anapata bado inatakiwa umakini kwenye uangalizi.

Ni mzunguko wa kwanza wenye ushindani mkubwa kwa kila timu kuonyesha shauku ya kupata ushindi. Ipo wazi kwamba hakuna anayependa kupoteza mchezo na kasi inaonekana.

Kwa namna kasi ilivyo basi ni muhimu kwa waamuzi kwenda sawa katika maamuzi yao.  Sheria 17 za mpira zifuatwe kwa umakini kupunguza lawama na kelele ambazo hazina sababu.

Yale makosa ya kibinadamu muda wake ushagota mwisho kwa wakati huu muhimu umakini. Waamuzi wanafanya kazi kubwa hilo lipo wazi.

Ukubwa wa kazi yao utaongezeka thamani pale wanapoendelea kutenda haki. Makosa yapo lakini yanaweza kupunguzwa na kuachwa kabisa.

Wachezaji wanapokuwa uwanjani ni muhimu kufuata sheria na kuacha ujanja ili wapate manufaa pia. Maamuzi yakiwa ya haki na wachezaji wakicheza kwa umakini kutakuwa na mwendo mzuri kwenye maamuzi.

Hakuna anayependa kuona maamuzi mabaya yanakuwa upande wake, hivyo hata waamuzi nao wanapenda iwe hivyo.

Kwa mechi zinazoendelea ni muhimu wamuzi kushirikiana kwa umakini na kuendeleza ile kasi ambayo wanayo kwa sasa.

Kasi hiyo ikipungua ligi itakuwa mbovu na ule ushindani nao utayeyuka kwa kuwa kuna timu zinaonekana kupendelewa muda huo haupo ni muda wa kufanya kazi kwa umakini.

NB: PICHA haina uhusiano na makala haya.