FULL MKOKO WA GAMONDI KUSAKA POINTI TATU ZA GEITA

MIGUE Gamondi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Geita Gold ameanzisha kikosi kazi kamili kusaka pointi tatu mbele ya Geita Gold.

Kwenye mchezo wa nne, ubao wa Uwanja wa Highland Estate ulisoma Ihefu 2-1 Yanga ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa Yanga kupoteza msimu wa 2023/24.

Kulikuwa na mabadiliko kikosi cha kwanza ambapo wachezaji waliopewa nafasi ni wale ambao walikuwa hawajaanza kwenye mechi zilizopita.

Leo Gamondi kaanza na jeshi kamili ikiwa ni pamoja na Djigui Diarra langoni.

Mbali na Diarra yupo Yao, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto ambaye ni nahodha.

Maxi Nzengeli, Clement Mzize, Aziz KI na Pacome Zouzoua wameanza kikosi cha kwanza Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.