Skip to content
UWANJA wa CCM Kirumba ubao unasoma Geita Gold 0- 3 Yanga ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Ni dakika ya 44 Pacome Zouzoa alianza kupachika bao na lile la pili ni mali ya Aziz KI dakika ya 45.
Mpaka mapumziko kwenye mchezo huo wa mpira uliokuwa na ushindani mkubwa Yanga walikuwa wanashambulia kwa kasi lango la Geita Gold.
Geita Gold walianza kwa kujilinda zaidi dhidi ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Ndani ya dakika mbili Geita Gold wameruhusu mabao mawili wakiwa nyumbani dhidi ya Yanga mchezo wa ligi.
Ni Maxi Nzengeli yeye alipachika bao la tatu kwenye mchezo huo dakika ya 68..