AZAM FC WAKOMBA POINTI MKWAKWANI, FEI AWAKA

WAKIWA ugenini, Azam FC imekomba pointi tatu mazima dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Bao la ushindi limefungwa na Feisal Salum, dakika ya 45 kwa pigo akiwa ndani ya 18 kutokana na makosa ya safu ya ulinzi ya Coastal Union.

Ni bao la nne kwa Fei Toto ambaye alifungua akaunti ya mabao kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Tabora United.

Ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Azam FC. Timu hiyo inaongoza ligi ikiwa na pointi 13 kibindoni baada ya kucheza mechi tano za ligi.

Namba mbili ni Simba wenye pointi 12 huku Yanga ikifuata nafasi ya tatu na pointi ni tisa.