Skip to content
SINGIDA Fountain Gate imefanikiwa malengo ya kusaka pointi tatu kwa msimu wa 2023/24 ikiwa Uwanja wa Manungu.
Katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Manungu dakika 90 zilikuwa upande wa Singida Fountain Gate waliopata ushindi.
Dakika 90 ubao umesoma Mtibwa Sugar 0-1 Singida Fountain Gate bao pekee ma ushindi likifungwa na Elvis Rupia dakika ya 43.
Kwenye mechi tatu ambazo Singida Fountain Gate ilicheza ilikuwa bado haijaambulia ushindi kwenye ligi.
Huu unakuwa ni mwanzo kwa kupata ushindi kwa timu hiyo ambayo ilitoka kwenye hatua ya Kombe la Shirikisho kwa kuondolewana Futere ya Misri.