BAADA YA DROO CAF, SIMBA WAJA NA NENO HILI

TAYARI Simba wamewatambua wapinzani wao watakaokutana nao kwenye mechi za kimataifa hatua ya makundi.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira imepangwa kundi B ambapo inasaka nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Droo hiyo imechezwa leo Oktoba 6, Afrika Kusini na Simba wameweka wazi kuwa malengo yao ni kupata matokeo kwenye mechi zao za kimataifa.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema malengo makubwa ni kutinga hatua ya robo fainali.

“Baada ya kuona wapinzani wetu na timu ambazo tutacheza nao hatuna mashaka ni maandalizi kwa ajili ya mechi hizo ambazo zitafanyika hivi karibuni.

“Tumeliona kundi letu namna lilivyo na tuna wachezaji bora pamoja na benchi la ufundi lenye mbinu hivyo tukutane Robo Fainali,”.

Kundi la Simba lina timu hizi:-Simba, Wydad, Jwaneng Galaxy na
Asec Mimosas.