SOKOINE MBEYA: PRISONS 1-3 SIMBA

UBAO wa Uwanja wa Sokoine, Mbeya umesoma Tanzania Prisons 1-2 Simba.

Edwin Balua alianza kumtungua Ally Salim dakika ya 16 kwa pigo la faulo kisha Clatous Chama aliweka usawa dakika ya 34.

John Bocco amepachika bao dakika ya 45 akiwa ndani ya 18.

Katika mwendo wa kawaida mastaa wa Tanzania Prisons walionekana wamenyoosha mikono kuonyesha kuwa Bocco alikuwa ameotea.

Ngoma iliporudi pili ambapo kila timu inapambana kusaka pointi tatu muhimu.

Ni Simba wameibuka na ushindi kwa bao la tatu kufungwa na Saido Ntibanzokiza kwa pigo la penalti.