SIMBA YAKOMBA POINTI TATU ZA WAJELAJELA

SAIDO Ntibanzokiza, kiungo mshambuliaji wa Simba amefungua akaunti ya mabao kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sokoine umesoma Tanzania Prisons 1-3 Simba.

Ni Edwin Balua kwa Prisons alianza kufunga dakika ya 16, Clatous Chama dakika ya 34 alipachika bao la kwanza kisha John Bocco bao la pili dakika ya 45.

Kete ya kufungia hesabu kwa Simba imepachikwa na Saido dakika ya 86 kwa pigo la penalti.

Ni namba moja kwenye msimamo Simba ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi 4.

Pointi tatu za wajelajela ugenini Simba wamekomba na kushinda mchezo wa nne kwenye ligi msimu wa 2023/24.