HUYU HAPA MCHEZAJI BORA NA KOCHA BORA WA LIGI KUU BARA

NI Waziri Junior nyota wa KMC ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa Septemba akiwashinda Jean Baleke wa Simba na John Nakibinge wa Tabora United.

Junior katupia mabao mawili muhimu ndani ya KMC na timu hiyo ilipata pointi sita dhidi ya JKT Tanzania na Geita Gold.

Pia kocha bora wa Septemba kwa mujibu wa Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), ni Abdihamid Moalin wa KMC.

Kocha huyo amewashinda Roberto Oliveira wa Simba na Abdallah Mohamed, (Bares) wa Mashujaa.

Pia ni Amir Juma kachaguliwa na kamati kuwa meneja bora wa Uwanja wa Azam Complex.