AZAM FC KWENYE KIGINGI KINGINE TENA

MATAJIRI wa Dar, Azam FC ni bandika bandua ugenini kwenye msako wa pointi sita muhimu katika mechi za Ligi Kuu Bara.

Kete ya kwanza ugenini kwa Azam FC ilikuwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na kete ya pili ni Tanga dhidi ya Coastal Union, Oktoba 6 Uwanja wa Mkwakwani.

Mchezo wa kwanza walitoshana nguvu kwa kugawana pointi mojamoja huku Yannic Bangala akipata maumivu hivyo hatakuwa kwenye mpango wa mchezo dhidi ya Coastal Union.

Katika mechi hizo Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Yussuph Dabo haitakuwa na muaji anayetabasamu Prince Dube kwa kuwa bado hajawa fiti pamoja na Yahya Zayd watakaokuwa nje kwa muda wa wiki tatu.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa mpango mkubwa ni kupata matokeo kwenye mechi watakazocheza.

“Kwa sasa nguvu kubwa ni kwenye mechi zetu za ligi ambazo tunacheza, kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu na hilo linawezekana kutokana na wachezaji kuwa na nia ya kupata ushindi,”.

Kwenye msafara wa Azam FC ulioibukia Tanga miongoni mwa wachezaji waliopo kwenue kikosi hicho ni pamoja na Idd Suleiman, Feisal Salum, Mbombo.