WAKIWA katika maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons Oktoba 5, tatizo la ubora wa wachezaji wa Simba limeanza kuwatesa mapema.
Wapo baadhi ya wachezaji hawana nafasi kabisa kikosi cha kwanza ikiwa ni pamoja na Chilunda hii ni kutokana na kutokuwa fiti, Henock Inonga, Aubin Kramo na Aishi Manula.
Luis Miqussone hakuwa fiti katika mchezo dhidi ya Power Dynamos, Azam Complex na hakuwa kwenye mpango kazi kabisa.
Benchi la ufundi la Simba chini ya Kocha Mkuu, Robert Oliveira linakazi ya kuwatumia kwa umakini wachezaji waliopo na wale ambao hawapati nafasi inabidi waanze kuzoea mfumo ambao bado haujajibu.
Simba imetinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa faida ya kupata mabao ugenini dhidi ya Power Dynamos kwenye mchezo wa kwanza ambapo ubao ulisoma Power Dynamos 2-2 Simba.
Mchezo wa pili ubao ulisoma Simba 1-1 Power Dynamos ambapo wachezaji wa Simba kipindi cha kwanza walicheza chini ya kiwango kilichozoeleka.
Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ameweka wazi kuwa walikutana na timu ngumu ambayo walishindwa kupata ushindi kwenye mechi zote mbili.
“Wapinzani wetu walikuwa imara na timu ambayo tulikwama kupata matokeo kwenye mechi zote mbili. Pia kushindwa kutumia nafasi ambazo tulizipata ilikuwa ni sababu ya kuwa hapa,”.