YANGA HAWAJAPOTEZA MKWAKWANI, TANGA

YANGA kwenye mechi mbili walizocheza Uwanja wa Mkwakwani hivi karibuni hawajapoteza hata mmoja.

Ilikuwa ni fainali ya Azam Sports Federation dhidi ya Azam FC, kwenye mchezo huo Yanga walishinda bao 1-0.

Mchezo wa pili kwa Yanga ilikuwa dhidi ya Azam FC katika hatua ya nusu fainali ya kwanza ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkwakwani.

Kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ni ushindi wa mabao 2-0 Azam FC, Uwanja wa Mkwakwani walipata Yanga.

Katika mechi mbili ambazo Yanga imecheza imekusanya mabao matatu ndani ya dakika 90 ikiwa haijapoteza.

Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi raia wa Argentina ambaye ni mrithi wa mikoba ya Nasreddine Nabi.

Gamondi amesema kuwa anatambua mchezo wa leo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa.

“Tunatambua mchezo wetu dhidi ya Simba utakuwa na ushindani mkubwa lakini tupo tayari,”.