SIMBA WANA ZALI NA MKWAKWANI

KATIKA mechi mbili za hivi karibuni ambazo Simba ilicheza Uwanja wa Mkwakwani, Tanga haijapoteza.

Simba imekuwa na zali ndani ya dakika 90 kutopoteza kwenye mechi za ushindani ambazo walicheza na leo wana kazi ya kufanya dhidi ya Yanga.

Ni Kariakoo Dabi ndani ya Tanga inatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku ambapo Yanga na Simba zote zimeweka wazi kuwa zipo tayari kwa ushindani.

Kwenye mechi ambazo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roerto oliveira ilicheza ilikuwa mzunguko wa kwanza mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union ambapo ubao ulisoma Coastal Union 0-3 Simba.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo huo Moses Phiri alipachika bao moja kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na Shomari Kapombe.

Mchezo wa pili ni nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate Agosti 10.

Ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ulisoma Simba 0-0 Singida Fountain Gate na Simba ilishinda kwa penalti 4-2.

Leo Agosti 13 Yanga v Simba fainali Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkwakwani.

Oliveira amesema :”Tupo tayari kwa mchezo wetu na wachezaji wapo tayari,”.