UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 kutokana na maandalizi ambayo wamefanya.
Timu hiyo yenye maskani yake Kinondoni mchezo wake wa kwanza kwenye ligi takuwa dhidi ya Yanga.
Ikumbukwe kwamba Yanga ni mabingwa watetezi wa ligi baada ya kutwaa taji hilo msimu wa 2022/23.
Timu hiyo inaendelea hiyo na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24 unaotarajiwa kuanza Agosti 15,2023. Kabla ya ligi kuanza ni Ngao ya Jamii inachezwa ambapo timu nne zinashiriki.
Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema: “Hatuna majeruhi katika kikosi chetu na tuna matumaini makubwa na wachezaji tuliowasajili katika kikosi chetu, tutaenda kufanya vizuri katika msimu mpya wa ligi.
“Tumeona ratiba tumepangwa na Yanga tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo chanya hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.