JESHI LA SIMBA DHIDI YA SINGIDA FOUNTAIN GATE

IKIWA ni mchezo wa nusu fainali ya pili Ngao ya Jamii ni mchezo kati ya Simba dhidi ya Singida Fountain Gate.

Mshindi wa mchezo wa leo Agosti 10 anakwenda kukutana na Yanga iliyotangulia kwa kupata ushindi dhidi ya Azam FC.

Fainali inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Agosti 13, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Langoni ni Ally Salim ulinzi ni Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Che Malone na Henock Inonga.

Viungo ni Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, Saido Ntibanzokoza,Kibu Dennis na Willy Onana kwa upande wa uahambuliaji sawa na Jean Baleke.

Yanga ilipata mabao yote mawili kipindi cha pili kwenye mchezo wao wa fainali ya kwanza.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Aziz KI na Clement Mzize.