WASIO NA TIKETI WAPEWA TAHADHARI HII SIMBA DAY

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa kwa wale ambao hawana tiketi za Simba Day ni muhimu kubaki nyumbani au wasifike maeneo ya Uwanja wa Mkapa.

Agosti 6 ni kilele cha Simba Day ikiwa ni siku maalumu ya utambulisho wa benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa Simba.

Tayari watani zao wa jadi Yanga wamekamilisha Wiki ya Mwananchi iliyopewa jina la SportPesa Wiki ya Mwananchi kisha Singida Fountain Gate ilikuwa ni Singida Big Day.

Matamasha yote hayo kuanzia lile la Yanga na Singida ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji na benchi la ufundi kwa msimu mpya wa 2023/24 unaotarajia kuanza Agosti 15.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimetolewa na Simba zimeeleza kuwa tiketi zimeisha kwa ajili ya wale ambao watahitaji kushuhudia burudani na utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa kwenye kikosi msimu wa 2022/23.

“Tunawasisitiza wale wote ambao hawajanunua tiketi kabisa wasisogee eneo la Uwanja wa Benjamin Mkapa. Kama huna tiketi kaa nyumbani Jeshi la Polisi Iinasisitiza ili kupunguza usumbufu usio wa lazima. Ambao hawana tiketi wanaweza kufatilia kupitia Azam TV, “.

Kwenye tamasha la Simba Day mgeni rasmi anatarajiwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu.