HAFIZ Konkoni mshambuliaji mpya wa Yanga amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/24.
Nyota huyo anatajwa kuwa mbadala wa mshambuliaji Fiston Mayele ambaye amesepa Yanga na kuelekea kupata changamoto mpya ndani ya Pyramids ya Misri.
Mayele ameweka wazi kuwa anaamini wachezaji wapya ambao wapo ndani ya kikosi cha Yanga pamoja na wale ambao walikuwa pamoja msimu wa 2022/23 watafanya vizuri.
Mshambuliaji huyo mpya raia wa Ghana amesema: “Natambua ushindani ni mkubwa lakini tutashirikiana na wachezaji wengine kupata matokeo tupo tayari.