AZAM FC wamezidi kuongeza makali yao kwa ajili ya msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Moto wao hauzimi ikiwa ni kasi juu ya kasi baada ya kutoka Tunisia ambapo waliweka kambi ya muda.
Kwa msimu wa 2022/23 Azam FC ilipishana na ubingwa wa ligi ambao ni Yanga walitwaa taji hilo na walipokutana na Yanga katika fainali ya Azam Sports Federation walipoteza kwa kufungwa ao 1-0.
Fainali hiyo dhidi ya Yanga ilikuwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga na mtupiaji kwa Yanga alikuwa ni Kennedy Musonda.
Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu Bara na mashindano ya kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24 ilipata ushindi kwenye mchezo wa kirafiki.
Mchezo huo ulikuwa dhidi ya Bandari FC ilipopata ushindi wa mabao 2-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Agosti 5.
Ni Sidibe na Dube hawa walikuwa wafungaji kwa Azam FC ambayo mchezo wake ujao ni wa Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali dhidi ya Yanga Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Yanga msimu wa 2022/23 walitwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa.