NYOTA mpya ndani ya kikosi cha Yanga Maxi Zengeli ameweka wazi kuwa yeye sio mtu wa ahadi bali kazi itaongea zaidi uwanjani.
Nzengeli ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Ni FC Maniema alikuwa akikipiga raia huyo wa DR Congo anavaa jezi namba 7 mgongoni kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kupanda na kushuka akiwa uwanjani.
Mchezo wake wa kwanza wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs kwenye Wiki ya Mwananchi alionyesha ujuzi wake na alitoa pasi moja ya bao kwa Kennedy Musonda.
Nyota huyo amesema: “Mimi sipendi kutoa ahadi kuhusu kile ambacho nitakifanya bali ninapenda kuona kazi ikiongea zaidi, mashabiki wasiwe na presha,”.
Yanga inakibarua cha kusaka ushindi kwenye Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Agosti 9 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Katika mazoezi yanayoendelea AVIC Town nyota huyo ni miongoni mwa wale wanaoendelea kujiandaa kwa msimu mpya wa 2023/24.