SINGIDA FOUNTAIN GATE WAFANYA KWELI

SINGIDA Big Day 2023 imefana kutokana na mpangilio wa matukio na mashabiki kujitokeza kushuhudia burudani.

Singida Fountain Gate wamefanya kweli kwa kupindua meza kibabe kwenye mchezo wao uliokuwa ukisubiriwa kwa shauku kubwa.

Katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki ubao baada ya dakila 90 umesoma Singida Fountain Gate 2-1 AS Vita.

AS Vita kutoka DR Congo walianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 3 kupitia kwa Ngoma Manianga.

Singida Fountain Gate hawakuwa wanyonge waliweka usawa dakika ya 20 kupitia kwa Malouf Tchakei na ngoma ya tatu mtupiaji ni Dickson Ambundo dakika ya 43.

Mbali na burudani ya mpira pia wasanii walipanda jukwaani ikiwa ni pamoja na Dulla Makabila, Nandy African Princess.