SINGIDA Fountain Gate hawataki mchezo kuanza msimu mpya na bonge moja ya basi mpya kabisa.
Ikumbukwe kwamba Agosti 2 2023 ni Singida Big Day Uwanja wa Liti mbali na kutambulishwa kwa kikosi kipya wametambulisha na basi jipya pia
Singida Fountain Gate msimu wa 2023/24 inaipeperusha bendera anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika.
Ni kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu Bara NBC wamewakabidhi Singida Fountain Gate.
Shughuli ya kukabidhiwa basi jipya la Singida Fountain Gate imefanyika Uwanja wa Liti.