FISTON Mayele amepewa jezi namba 9 ndani ya kikosi cha Pyramids ikiwa ni ingizo jipya.
Nyota huyo msimu wa 2022/23 alikuwa ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kilikuwa kinanolewa na Nasreddine Nabi.
Namba 9 inakuwa ni zawadi kwake Mayele kuendelea kuitumia kama alivyokuwa akifanya ndani ya Yanga na sasa atakuwa akiivaa mbele ya Waarabu hao wa Misri.
Ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Yanga msimu wa 2022/23 alipotupia mabao 17.
Mbali na kusepa na tuzo ya ufungaji bora alitwaa tuzo ya mchezaji bora na jina lake lilikuwa kwenye orodha ya kikosi bora.
Anaanza changamoto mpya ndani ya kikosi cha Pyramids akibainisha kuwa anakwenda kuanza changamoto mpya.
Mayele amesema anawashukuru Yanga na mashabiki kwa ajili ya sapoti ambayo wamempa ndani ya timu hiyo.