MTIBWA SUGAR WAMEANZA KAZI

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umebainisha kuwa haujamaliza kazi ya kutambulisha nyota wapya kutokana na kujipanga kuwa tofauti.

Timu hiyo imeweka kambi Morogoro kwenye Uwanja wa Manungu na jana ilitarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC, Uwanja wa jamhuri.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa walikuwa kimya kwa muda wakikamilisha utaratibu wa kuwasajili wachezaji wenye ubora.

“Tumerejea baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu wengi wakadhani hatutafanya jambo tumeanza na kazi bado ipo kwa kuwa usajili wetu ni mzuri na unazingatia mahitaji muhimu.

“Itoshe kusema kwamba Mtibwa Sugar ni chuo cha mpira kuna vijana wenye uwezo mkubwa wametoka kutwaa ubingwa wa ligi ya vijana wapo ambao watapanda na wengine tutawaleta wenye uzoefu,” amesema Kifaru.

Mtibwa Sugar imewatambulisha baadhi ya wachezaji wapya ikiwa ni Juma Luizio, Yassin Mustapha kwa ajili ya msimu mpya.