MATOKEO MAZURI NA MABAYA YANATAFUTWA UWANJANI

USHINDANI kwa msimu mpya unategemewa na maandalizi ya ambayo yanafanywa kwa wakati huu kwa kila timu.

Iwe ni Yanga ama Singida Fountain Gate hata Simba au Namungo wote matokeo yanaamuliwa na kile wanachokifanya kwa sasa.

Kila timu inapambana kwa ajili ya maandalizi huku mabingwa watetezi Yanga kambi yao ikiwa AVIC Town Kigamboni, Singida Fountain Gate ni pale Arusha.

Azam ni Tunisia huku Simba wakiwa wameweka kambi Uturuki yote kheri.

Muhimu kila mmoja kuhakikisha anatimiza wajibu wake kwa umakini na muda uliopo ni sasa hakuna ambaye anapenda kupata matokeo mabaya.

Matokeo mabaya yanapatikana ndani ya dakika 90 sawa na yale mazuri ambayo yanapatikana kwa timu itakayofanya maandalizi mazuri.

Ipo wazi kwamba mchezo wa mpira sio mchezo wa kujificha kila kitu kinaonekana uwanjani hilo ni muhimu kufanyiwa kazi muda uliopo.

Kuanzia kwa wachezaji ni muhimu kuwa tayari kwenye muda wa maandalizi hiyo itawaongezea hali ya kujiamini na nguvu ya kupambana kwenye kutafuta matokeo.

Furaha ya mashabiki ipo kwenye matokeo mazuri ambayo yanapatikana uwanjani hivyo kwa kutimiza majukumu kwa umakini kunaongeza nguvu ya mashabiki kuzidi kujitokeza uwanjani.

Hamasa kubwa ambayo inafanyika kwa mashabiki itakuwa endelevu ikiwa matokeo yatakuwa yanapatikana uwanjani kutoka kwa wachezaji.

Mchezo wa makosa unahitaji umakini kwenye kutendea kazi katika kila hatua ambayo inakuwa inafanyika kwenye uwanja wa mazoezi.

Nidhamu kwa wachezaji nje na ndani ya uwanja ni nguzo kubwa katika kupata matokeo mazuri ambayo yataongeza thamani ya wachezaji nje na ndani ya uwanja.

Kikubwa kwa benchi la ufundi ni kuwapa mbinu imara wachezaji na kutambua namna ya kwenda nao sawa pasipo upendeleo na kuongea nao pale wanapokosea.

Haina maana kwa kuwa ni mchezaji mwenye uwezo basi kila mechi ataanza yeye ama atakuwa anakwenda kinyume na utaratibu husika hiyo sio sawa.