VIDEO:ISHU YA BANGALA KUIBUKIA AZAM FC NENO KUTOKA YANGA

JULAI 29 kiraka ndani ya kikosi cha Yanga, Yannick Bangala ametangazwa kuwa ni mali ya Azam FC.Bangala mkataba wake na Yanga ulibaki wa kadanrasi ya mwaka mmoja ambapo ulitarajiwa kugota mwisho 2024.

Taarifa iliyotolewa na Yanga imeeleza kuwa wamefikia makubaliano mazuri na Azam FC ambao wamebainisha kuwa wamefikia makubaliano ya kumnunua mchezaji huyo kutoka Yanga.

Ni kandarasi ya miaka miwili amesaini baada ya kupima afya ndani ya Azam FC.