MTIBWA SUGAR WAMEANZA BALAA LAO

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeanza kushusha vyuma vya kazi kwa ajili ya msimu mpya ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mtibwa Sugar ni miongoni mwa timu ambazo zimetoa wachezaji bora ambao wanacheza ndani ya Yanga, Singida Big Stars, Azam FC.

Kwa msimu wa 2023/24 Singida Big Stars itakuwa inaitwa Singida Fountain Gate.

Wapo pia ambao waliwahi kupita ndani ya Simba na ni timu yenye nguvu kwa upande wa vijana ikiwazidi wakongwe Yanga, Simba katika uwekezaji.

Ni Pascal Kitenge, Issa Rashid (baba ubaya) na Caspian Ponera hawa awatakuwa ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar msimu wa 2023/24.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa msimu mpya watakuwa na kikosi imara kitakachokuwa na maingizo mapya ya wachezaji bora.

“Tunafanya usajili makini na tuna vijana ambao tutawapandisha kutoka kwenye timu yetu ya U 20, hapo wapo kama sita hivi watacheza timu ya wakubwa.

wamepandisha zaidi ya vijana sita toka kikosi cha U20 ambacho kilichukua ubingwa mbele ya Geita Gold.

“Wapo wachezaji wapya ambao tutakuwa nao kwenye kikosi ikiwa Juma Luizio, Kelvin Nashon, Mohamed Kassimu Ally na Omar Ally Marungu huyu ilikuwa ni kutoka U 20,” amesema Kifaru.

Mtibwa Sugar imeweka kambi Morogoro na inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC.