KOCHA SIMBA AANZA KAZI ZANZIBAR

 MASSOUD Djuma raia wa Burundi ameanza rasmi kazi ndani ya Klabu ya KMKM ya Zanzibar kwa ajili ya kuinoa timu hiyo kwa msimu wa 2023/24.

Djuma aliwahi kuifundisha Simba inayoshiriki ligi ya Tanzania pia aliwahi kuifundisha Dodoma Jiji kwa sasa yupo ndani ya KMKM akichukua mikoba ya Hemed Morocco ambapo timu hiyo inashiriki mashindano ya kimataifa.

Timu nyingine kutoka Tanzania Bara ambazo zinashiriki mashindano ya kimataifa ni Singida Fountain Gate ambayo ni msimu wake wa kwanza kwenye anga la kimataifa.

Singida Fountain Gate kwenye Kombe la Shirikisho sawa na Azam FC huku Yanga na Simba hizi zitakuwa ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ikumbukwe kwamba Morocco aliyekiongoza kikosi hicho kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar yupo na timu ya Geita Gold iliyokuwa inanolewa na Felix Minziro atakayekuwa ndani ya Tanzania Prisons.

Djuma Julai 28 alianza rasmi kuwapa mbinu wachezaji wake ikiwa ni maandalizi ya timu hiyo kwenye mashindano ya ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hiyo inatarajiwa kumenyana na Saint George ya Ethipia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Agosti 18-20.