KOCHA YANGA ATAMBULISHWA NAMUNGO

CEDRICK Kaze aliyekuwa kocha msaidizi wa Yanga kwa sasa atakuwa Kocha Mkuu Namungo FC.

Kaze alipewa mkono wa asante ndani ya Yanga baada ya msimu wa 2022/23 kugota mwisho.

Sasa anaibukia ndani ya Namungo FC inayoshiriki Ligi Kuu Bara hivyo atakuwa na nafasi ya kukutana na waajiri wake wa zamani Yanga kwenye mechi za ushindani.

Ndani ya Namungo ambapo ametambulishwa Julai 24 atashirikiana na Dennis Kitambi na Shadrack Nsajigwa kukiongoza kikosi cha Namungo.

Tayari kikosi cha Namungo kimeanza maandalizi kuelekea msimu wa 2023/24 ambapo kina nyota wapya ikiwa ni pamoja na Erasto Nyoni.

Mkongwe Nyoni alikuwa ndani ya kikosi cha Simba kabla ya kukutana na Thank You hivyo kwa sasa yupo Namungo.