HATIMAE SportPesa Wiki ya Mwananchi 2023 imeenda na kweli imekuwa hivyo kwa namna ambavyo walikuwa wamepanga.
Mpangilio mzima wa matukio na namna ambavyo mashabiki walijitokeza kuona burudani hizo.
Hatua moja kila wakati mbali na mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao ulikamilika kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 1-0 Kaizez Chiefs bado kazi imeonekana.
Sio jambo dogo ambalo Yanga wamefanya na wanapaswa kuendelea kufanya maboresho zaidi kwa nyakati nyingine.
Mapungufu hayawezi kukosekana kwenye shughuli kubwa kama hiyo hivyo muhimu pale ambapo kumeonekana kuna mapungufu lazima yafanyiwe kazi.
Kwa mashabiki mnastahili pongezi kwa namna ambavyo mmejitoa kuishangilia timu mapema kabisa wengi walianza kujitokeza Uwanja wa Mkapa.
Wachezaji tumeona mbali na Kennedy Musonda kufunga bao dakika ya 45 akitumia pasi ya Maxi ilikuwa ni burudani tu hivyo basi ni mwendelezo mzuri ikiwa ubora utaendelea.
Wachezaji wanaanza kutambua namna ambavyo mechi kubwa za kimataifa zinakuwa hii ni kuendelea kujijenga zaidi.
Serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikifuatilia na kutekeleza mipango ya maendeleo ya mpira Tanzania hili nalo ni kubwa hivyo ni mwanzo wa msimu mpya mipango makini inahitajika.
Umeonekana uwezo wa washambuliaji wazawa ikiwa ni Clement Mzize na Ngushi wanapaswa kuwa na mwendelezo bora kwa ajili ya ushindani wa namba na kutimiza majukumu yao.