HATIMAE ni leo ni siku ya SportPesa Wiki ya Mwananchi, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni maalumu kwa ajili ya Yanga na mashaiki wa mpira duniani kote.
Yanga itakuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/24.
Unasikia hii imeendaaa, ni kauli mbio inayatumiwa na Yanga kwa msimu huu katika kukamilisha mpango kazi wenye hesabu nyingi.
Ikumbukwe kwamba Yanga ni mabingwa wa ligi msimu wa 2022/23 hizi ni hesabu za kwenda kupambania kwa mara nyingine msimu wa 2023/24.
Ni burudani za kutosha zinatarajiwa kuwa Uwanja wa Mkapa ikiwa ni pamoja na show kutoka kwa wasanii mbalimbali kwenye kila sekta movie, muziki, sarakasi mpaka ngonjera yote yapo kwa Wananchi.
Utambululisho wa benchi jipya pamoja na wachezaji ni miongoni mwa yale ambayo yatafanyika na mwisho ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Saa 1:00 usiku mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ikiwa ni burudani inayosubiriwa kwa wingi kutoka kwa mashabiki wa Yanga na Kaizer Chiefs.
Jezi namba sita wa Yanga Skudu naye yupo amebainisha kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Kaizer Chiefs ambao utakuwa na ushindani mkubwa.
Kila la Kheri Yanga kwenye Wiki ya Mwananchi ikawe na mafanikio na hatua nyingine zaidi ziendelee kila wakati.